Simba yaendelea kung'ara ligi kuu ikiichapa Kagera 2-0.


Timu ya Simba imeendelea kutoa shangwe kwa mashabiki wake baada ya kuitwanga Kagera Sugar bao 2-0 kwenye uwanja wa Taifa.

Kiungo mshambuliaji wa Simba Shiza Kichuya ameendelea kuwa gumzo baada ya kufunga bao lake
saba kwa mkwaju wa penati leo akizidi kuiongoza vema timu yake katika kila ushindi.

Simba imecheza mechi 9 hadi sasa ikiwa imekusanya jumla ya pointi 23 na kuendelea kusimama kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom.

Mbali na bao hilo la Shiza Kichuya pia Kiungo Mzamiru Yasin ameifungia timu yake bao la kwanza tangu aliposajiliwa na Simba akitokea Mtibwa Sugar.


Comments