Timu ya Simba kupitia msemaji wake Haji Manara imeiomba serikali iwasamehe ili kuondokana na adhabu ya kufungiwa kutumia uwanja wa taifa kutokana na vurugu za mashabiki wao katika mtanange wa watani wa jadi.
Uongozi wa timu hiyo umeanza kwa kumtaka radhi Rais Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli pamoja na waziri husika wa wizara hiyo Nape Nnaye pamoja na TFF kuwafikiria kwa mara nyingine kutumia uwanja huo.
Simba kupitia Haji Manara walisema kuwa wanatoa ahadi ya kuwa jambo hilo halitajirudia tena kwenye mechi yao ikiwa ni pamoja na kuitaka TFF kutafuta waamuzi wa kimataifa kwenye pambano la Simba na Yanga ili kuepusha migogoro uwanjani.
"Tunaomba radhi kwa Muheshiwa Rais John Magufuli, na serikali yake kwa ujumla, Waziri husika pamoja na TFF kwa kile ambacho kilifanywa na mashabiki, tunaahid kuwa jambo hili halitajirudia kwa mara nyingine.
"Vilevile TFF katika pambano lingine la Simba na Yanga itutafutie mwamuzi kutoka nje ya nchi ya Tanzania sisi tupo tayari kugharamia." Alisema Manara

Comments
Post a Comment