Simba, Yanga marufuku uwanja wa Taifa, Nape atoa tamko


Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Micheza Nape Nnauye amezifungia timu za Simba na Yanga kutumia uwanja wa taifa na kuzitaka timu zitafute viwanja vyao.

Nape alitoa tamko wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio liliotokea na jana kutokana na sitofahamu ya mashabiki wa Simba.

"Nadhani mmeona kilichotokea siku ya jana ni vitu vya makusudi ikiwa watu wanalipa kodi ya matangenezo ya uwanja.

"Nadhani Simba na Yanga wanaweza kutafuta viwanja vingine vya kutumia hadi hapo tutakapoamua kitu cha kufanya." Alisema Waziri

Adhabu hiyo imewakuta pia na Yanga kutokana na kujibu mapigo walipoamua kurusha viti uwanjani baada ya Shiza Kichuya kuchoma bao dakika ya 88.

Comments