Simba yazidi kupaa VPL, yaichapa Mwadui 3-0.


Timu ya Simba imeendelea kudhihirsha ubora wake msimu baada ya kuibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Mwadui.

Kiungo wa Simba Mohamed Ibrahimu ameibuka shujaa wa mchezo baada ya kutumbukiza nyavuni bao mbili na kutengeneza moja lililofungwa na Shiza Kichuya.

Ushindi huo unaiongoza Simba kileleni mwa msimamo wa ligi kuu baada ya kuzoa jumla ya pointi 32 katika michezo 11 ambayo imecheza ligi kuu hadi sasa.

Kwa upande wa matokeo ya mechi zingine African Lyon imevutana shati na Tanzania Prisons ambazo zimetoka 1-1, Mbeya city imeshinda bbao 3-1 dhidi ya Majimaji huku Toto ikiilaza Mtibwa Sugar bao 3-2 katika uwanja wa CCM Kirumba.

Comments