Stand utd yaiongezea machungu Azam, yaichapa 1-0.


Timu ya Stand united ya Shinyanga jana imemweka kocha Azam Zeben Hernandez kwenye hali ngumu baada ya kuifunga timu hiyo bao 1-0.

Stand ilipata bao la ushindi kupitia Adam Salamba ambaye alitokea benchi na kupeleka kilio kwa mabingwa hao wa Afrika Mashariki na kati.

 Majonzi yakiongezeka Azam ushindi huo ni furaha kwa Stand united ambao hawajapoteza mechi yoyote hadi sasa katika mechi za ligi.

Azam haijpata haijapata ushindi kwenye michezo minne ya mwisho iliyocheza hadi sasa baada ya kupoteza kwa Simba na Simba, pia ilitoka Sare na Ruvu Shooting na kupoteza jana dhidi ya Stand united.

Comments