Tegete awaonya Simba itakapotua Kambarage


Mshambuliaji wa Mwadui FC Jeryson Tegete ametamba kuifunga Simba timu hizo zitakapokutana katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga siku ya Jumapili.

Tegete ambaye amewahi kuifunga Simba mara nyingi alipokuwa na Yanga miaka kadhaa iliyopita ametamba kuendeleza rekodi yake ya kuiburuza Simba kila anapokutana nayo.

"Simba ijipange hakuna matokeo rahisi, timu yangu inahitaji pointi 6 ni lazima tuzipate, ni lazima nifunge goli.

"Tumeweka malengo kwamba ni lazima tupate ushindi na kuondoka na pointi 3 nadhani kila  kitu kinawezekana endapo tutaweka juhudi zetu katika ushindi." Alisema Tegete.

Comments