Toto Africans yafanya kweli chini ya kocha mpya, Yaiburuza kagera 2-0


Timu ya Toto Africans ambayo kwa sasa ipo chini kocha mpya Khalifan Ngasa jana imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera katika uwanja wa Kaitaba Kagera.

Hivi karibuni aliyekuwa kocha wa timu hiyo Rogasian Kaijage alibwaga manyaga baada ya kushindwa kujua uelekeo wa timu hiyo kutokana na matokeo mabovu kwenye ligi.

Tangu kutua kwa kocha Khalifan Ngasa aliahidi kuwa atabadilisha mambo kadhaa kwenye timu hiyo ikiwemo kuleta umoja kwa wachezaji jambo ambalo lilikosekana kwenye timu hiyo hapo awali.

Ushindi huo unaweza kurejesha matumaini mapya kwa Toto Africans ambayo huenda ikaendelea kupata matokeo mazuri kutokana hali mpya ya wachezaji kikosini.



Comments