Uamuzi wa Kaijage kuachana na Toto ni sahihi kabisa


Baada ya kufanya vibaya katika mechi za ligi kuu kocha wa Toto African Rogasian Kaijage ameamua kubwaga manyanga mwenyewe baada ya kuwasilisha barua ya kujiuzulu kuinoa timu hiyo.

Baada ya kufungwa bao 1-0 na Ndanda katika mechi ya mwisho kaijage hakuona haja ya kuendelea na timu hali ya kuwa haoni mweleko huenda akainyanyua timu hiyo.

Waswahili husema heri lawama kuliko fedheha, Binafsi naamunga mkono Kaijage ambaye kachukua uamuzi sahihi, nakumbuka wakati ule Remi Garde alipoichukua Aston Villa ambayo ilikuwa hoi baada ya kuinoa kwa miezi 5 kocha huyo alisalimu amri na kuachana na timu hiyo mwezi Machi mwaka huu.

Nadhani hakuna dhambi kujiuzulu ni suala zima la kulinda na kutunza vema wadhfa wako na hadhi yako. Ingawa Toto African imesheheni vijana wa kutosha nadhani kocha huyo ameshindwa kuwatumia vijana hao kwa usahihi, ameshidwa kuunda mfumo imara na kuweka mbinu hatarishi kwa ajili ya wapinzani wake.

Hakuna ubaya ikiwa ameacha nafasi hiyo wazi kwa ajili ya maendeleo ya Toto African ambao huenda wakapata kocha mwingine aliye bora zaidi kuliko Rogasian Kaijage. Watanzania tunatakiwa kujifunza jambo ikiwa tuna nafasi ya kuwapisha wengine basi tunatakiwa kufanya hivyo kwenye maisha yetu.

"Nadhani ni vizuri kufanya ukijua uelekeo wake, watanzania wengi huwa hatujui hili, katika mpira tuna uchungu wa matokeo na si uchungu wa kuiandaa team pamoja kuandaa matokeo bora." Alisema kaijage baada ya kuchukua uamuzi huo.

Kwa upande wangu hii kauli bora ya bora ya Kaijage nadhani watanzania tunatakiwa kufahamu ni jambo gani tunafanya kwenye maisha yetu ikiwemo na kufahamu mwelekeo wake pia, ipo haja ya kujifunza na kuchukua maamuzi sahihi katika yale tunayofanya.

Rogasian Kaijage yuko sawa, ameacha nafasi wazi kwa yule ambaye atafahamu uelekeo wa Toto African kulingana na aina ya wachezaji alionao, hakuna dhambi katika bali tujifunze uelekeo wa mambo na kuchukua uamuzi sahihi.

Comments