Ukata wazidi kuitafuna Ndanda FC


Timu ya Ndanda imesema kuwa huenda ikiajitoa kwenye mbio za kuendelea na ligi kuu kutokana na hali mbaya kiuchumi inayoikabili timu hiyo.

Habari za ndani kutoka kwenye timu hiyo zinaeleza kuwa timu hiyo imefikia kwenye hali mbaya kiasi cha kushindwa kuwalipa mishahara wachezaji wake.

Hivi karibuni Ndanda FC ilichelewa kutoka Mwanza kutoka na kukosa fedha za kulipia hotel ambapo iliwalazimu kulala maeneo ya dumila mkoani Morogoro na kushindwa kuingia Dar es Salaam moja kwa moja.

"Ni kweli tunakabiliwa na hali mbaya kiuchumi kiasi kwamba tumeshindwa kuwalipa wachezaji mishahara." Kilisema chanzo.

Comments