Mshambuliaji wa Taifa Stars Thomas Ulimwengu amegoma kupokea mkataba mpya TP Mazembe muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkabata wake.
Ulimwengu amegoma mkataba huo akiwa na malengo ya kuinuka kama Samatta ambaye alitimka na kwenda kujiunga na Klabu ya Genk ya Ubelgiji.
Nyota huyo ambaye amepata umaarufu mkubwa nchini Congo kutokana na kiwango chake bora amesema kwa sasa malengo yake ni kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
Ulimwengu ameweka wazi kuwa zipo baadhi ya timu barani Ulaya ambazo zimeonesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo..
"Kwa sasa sifikirii tena kucheza Afrika, kwa kuwa zipo baadhi ya barani Ulaya ambazo zinanihitaji na si muda mrefu kila kitu kitakuwa wazi." Alisema Ulimwengu.

Comments
Post a Comment