Mshambuliaji wa Taifa Stars Thomas Ulimwengu amerejea nchini kwa mapumziko baada ya kuachana na TP Mazembe ambapo atajiunga na timu ya Azam kwa ajili ya mazoezi.
Ulimwengu atapumzika wiki moja ambapo muda mfupi ataungana na Kikosi cha Azam kufanya mazoezi kabla ya kutimka Ulaya kuanza maisha mapya kwenye soka la ushindani.
Wakala wa mchezaji huyo Juma Kisongo amesema kuwa mchezaji hana nia kucheza katika timu za Simba na Yanga licha ya kuonesha jitahada za kutaka kupata huduma ya mchezaji huyo.
"Ulimwengu yupo Dar, atapumzika kwa wiki kwa kuwa bado anasumbuliwa na majeraha baada ya apo ataungana na Azam kwa mazoezi ili kujiweka fiti kwa ajili ya kusakata kabumbu barani Ulaya." Alisema Kasongo

Comments
Post a Comment