Kama ulikuwa hujui basi usajili uliofanywa na Simba msimu huu ndiyo unaowapa kiburi wababe hao wa mitaa ya Msimbazi kuburuza ligi kuu.
Jana Simba iliweza kupata ushindi wa bao moja dhidi ya Mbao FC ya Mwanza kupitia Mzamiru Yasin aliyefunga zikiwa zimesaria dakika 5 mpira kumalizika.
Matunda ya usajili katika klabu ya Simba yameanza kuonekana kupitia nyota wake waliosajili na timu hiyo msimu huu akiwemo Shiza kichuya, Mzamiru Yasini, Janvier Bokungu, Mohamed Ibrahimu na Laudit Mavugo.
Simba inaongoza kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa imekusanya jumla ya pointi 26 huku msahmbauliaji wake shiza kichuya akiwa amefunga magoli 7 hadi sasa na kuongoza katika orodha ya wachezaji.
Pia timu hiyo inajivunia wachezaji wa akiba ambao wamekuwa wakitokea benchi na kubadilisha matokeo kwenye timu hiyo akiwemo Mohamed Ibrahimu aliyesaliwa akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Comments
Post a Comment