Villa yamwondoa Di mateo


Uongozi wa timu Aston Villa umemwondoa rasmi kocha wa wao Di Matteo baada ya kupata ushindi mmoja katoka mecho 12 za kwanza.

Villa imefikia uamuzi huo baada ya Di Matteo kukosa ushindi katika mechi ya mwisho dhidi ya Preston North End ambapo ikiwa ugenini bao 2-0 zilitosha kukata matumaini ya uongozi huo kwa kocha huyo.

Kwa sasa kocha msaidizi wa timu hiyo Steve Clarke atashika timu hiyo kwa muda hadi uongozi wa timu itakapopitisha jina la kocha mpya ambaye atarithi rasmi kiti cha Di Matteo.

Di Matteo pia aliwahi kuzinoa baadhi ya timu England ikiwemo Blackpool, Chelsea ambako nako aliondolewa kutokana na matokeo mabaya.

Comments