Mechi kati ya Taifa Stars na Ethiopia ambayo ilitakiwa kuchezwa tarehe 8 ya mwezi imehairishwa kutokana na kuzuka kwa vurugu nchini.
Stars ilitakiwa kuelekea Addis Ababa kwa ajili kupiga mechi na taifa hilo lakini hali hatarishi iliyoibuka nchini humo imevunja matumaini ya watanzania na sasa mechi hiyo imehairishwa rasmi.
Kwa upande wa TFF katibu mkuu Selestine Mwesiga amesema kuwa wanaendelea na juhudi za kutafuta mechi nyingine kwa ajili ya kuipima nguvu Stars.
"Tunafanya juhudi kutafuta kutafuta mechi nyingine kwa hizi siku chache zilizobaki, endapo itashindikana tutamtaharifu kocha." Alisema Mwesiga

Comments
Post a Comment