Nakumbuka michuano ya kombe la mapinduzi ambayo kwa kawaida hufanyika mwezi January kule Zanzibar, moja ya mechi iliyonishangaza ni pale kichuya alipozamisha goli la ushindi dhidi ya Azam wakati huo akiwa na Mtibwa Sugar baada ya kuunganisha krosi sasa iliwekwa kwenye njia na Baba Ubaya.
Ingawa mwamuzi wa pembeni (line) alikataa goli na kusema kuwa Kichuya alikuwa ameotea nadhani ilimfanya mwamuzi wa kukataa lile hata kama aliamini kuwa ni goli.
Kwa mara nyingine makosa hayo yamejitokeza jana katika mechi ya Yanga na Simba, kabla ya kuzamishwa wavuni kwa goli la Amis Tambwe, Ajib alikuwa amefunga bao sahihi ambalo ni umakini ulikuwa mdogo kwa line ambaye alikataa bao la wazi na kuinyima Simba haki yao ya kuongoza.
Ingawa kimchezo Amis Tambwe alimzidi ujanja Novaty Lufunga wa Simba na kutumbukiza mpira wavuni na kuandika bao la kwanza Yanga, kiuhalisia kama mwanasoka ni lazma umpe Tambwe sifa yake kwa kumpa funzo beki ambaye anakosa umakini, lakini nilisikitishwa na kitendo cha mwamuzi wa pembeni na mwamuzi wa mchezo kushindwa kuona jinsi Tambwe alivyousapoti mpira kwa mkono wake na kufunga.
Nadhani kuna haja ya waamuzi kubadilika, na kurekebisha makosa yao, ingawa kimchezo mashabiki wa Simba walikosa uungwana pale walipofanya uharibifu wa kung'oa viti uwanjani, nadhani kwa waliokuwa makini huenda goli la Ajib lilikuwa chanzo kabla ya kufika kule kwa Tambwe.
Ingawa wingi wa mashabiki unaamini refa aliwapendelea Yanga kwa kumzawadia Tambwe ambaye alimuacha kiufundi beki wa Simba, lakini kwa waliofahamu nini maana ya kuotea chanzo cha tatizo kilianzia pale.
Binafsi naishukuru Azam Tv huwa najifunza mengi kupitia kipindi chao cha kipenga kila jumatano pale ambapo mwamuzi mzoefu Osman Kazi hufafanua zile sheria 17 za soka, wapi ilikuwa sahihi na wapi si sahihi nadhani tuna nafasi ya kujifunza kupitia wao endapo watatuelimisha jumatano ya wiki inayokuja.

Comments
Post a Comment