Kocha anayeinoa timu ya Mwadui ya Shinyanga Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema kuwa analazimika kuachana na soka la Tanzania kutokana na ukosefu wa waamuzi makini viwanjani.
Julio amekuwa akiwahatuhumu wahamuzi wa Tanzania kuwa hawatendi haki uwanjani hali inayopelekea matokeo mabovu kwa timu yake mara kadhaa.
"Nadhani mimi na soka, natangaza rasmi kuachana na soka la Tanzania kwa kuwa waamuzi hawatendi haki uwanjani, nadhani soka linachezwa kwa ajili ya kufurahisha watu waonekane uwanjani hata kama hawajui.
"Nimefundisha soka Qatar, Yemen na Dubai ambako kote uko sijawahi kushindwa nadhani lipo kundi kubwa la watu wanafanya mambo kumwaribia mtu mwingine." Alisema Julio.
Julio alipoteza mechi ya mwisho alipokaribishwa na Mbeya city katika uwanja wa Sokoine baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0.

Comments
Post a Comment