Wawa, Nyoni wapo kamili kuivaa Stand utd



Uongozi na mashabiki wa Azam huenda wakaanza kukenua meno baada ya majembe yao akiwemo Serge Wawa na Erasto Nyoni kurejea uwanjani.

Wawa na Nyoni walijumuishwa katika timu ya vijana ambayo walicheza mchezo wa kirafiki ambapo dakika 45 walizocheza walinzi hao zilitosha kutoa majibu kuwa wako fiti.

Wawa na Nyoni wameungana na Aggrey Moris Mazoezini ambaye na yeye alikuwa nje kutokana na majeraha lakini kwa ujumla wachezaji wote wanaonekana kurejea kwenye hali yao.

Wachezaji wapo fiti kusakata kabumbu katika mechi inayofuata dhidi ya Stand Utd ambayo haijapoteza mechi yoyote hadi sasa.

Comments