Kocha wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger amewataka wachezaji wao kujituma uwanjani ili kuamua hatma yao katika ligi ya England.
Wenger alizungumza hayo mapema katika mkutano na waandishi wa habari wakati Arsenal ikijandaa kuchuana na Middlesbrough katika mchezo ambao utachezwa kesho kwenye uwanja wa Emirates.
Wenger alisisitiza kuwa ni lazma timu hiyo ipambane na kujikwamua kwenye msitu mnene kwa kuwa kila adui anawatani kuwawinda kwenye eneo hilo.
"Tunaishi kwenye msitu mkubwa ambao kila mnyama anahitaji kututafuna, kuna haja ya kujilinda ili tuweze kuishi na huo ndiyo ushindani." Alisema Wenger
Arsenal imeendelea kufanya kwenye ligi ikiwa inachuana na Manchester city kwenye msimamo wa ligi kwa pamoja zikiwa na pointi 19.

Comments
Post a Comment