Washambuliaji wa Chelsea Willian pamoja na Diego Costa ndiyo waliombeba Conte baada ya kuzamisha nyavuni mabao ya ushindi wa Chelsea dhidi ya Hull city katika uwanja wa KCOM.
Chelsea walionekana kuchachamaa kipindi cha pili na kuanza kuzamisha magoli nyavuni kupitia Willian aliyefunga dakika 61 ya mchezo na Costa akashindilia msumali wa pili kunako dakika ya 67.
Kikosi cha Antonio conte kilionekana kuwa mabadiliko kidogo ambapo jana Branslav Ivanovic, Oscar pamoja Cesc Fabrigas hakuanza kwenye timu hiyo.
Chelsea imeibuka na pointi tatu baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo kutoka kwa Liverpool na Arsenal sasa imerejea kwenye nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na jumla ya pointi 13.

Comments
Post a Comment