Yanga hii hatari, yaichapa 6-2 Kagera


Timu ya Yanga imedhihirisha kwa vitendo kwamba bado ipo kwenye chati baada ya kuitandika Kagera Sugar bao 6-2 hapo jana katika uwanja wa Kaitaba.

Mabao mawili ya mshambuliaji Obrey Chirwa, Donald Ngoma, Deus kaseke na Simon Msuva yalitosha kuipa Yanga ushindi huo mnono ikiwa Ugenini.

Yanga ambayo imepoteza mechi moja hadi sasa walionekana kuwamudu vema kagera Sugar katika eneo la kati ambapo juhudi kubwa za Thaban Kamusoko pamoja na Haruna Niyonzima zilizaa matunda yalioizamisha Baharin Kagera.

Ushindi huo unaiongoza Yanga kuchanja mbuga na kuiacha Azam ikiendelea kuwa chini ya msimamo wa ligi kutokana na mfululizo wa magoli ya sare.

Comments