Yanga ruksa uwanja wa uhuru


Baada ya kufungiwa kutumia uwanja wa taifa na serikali hatimaye Yanga imepewa ruhusa ya kutumia uwanja wa uhuru kama mwenyeji kwenye ligi kuu.

Timu hiyo ilipeleka maombi yake TFF ambayo baada ya kujiridhisha imeamua kutoa ridhaa kwa wanajangwani hao kutumia uwanja huo.

Mechi za ligi kuu zitaendelea siku ya jumatano ambapo Yanga itaikaribisha Mtibwa Sugar katika uwanja wa Uhuru.

Mbali na mechi hiyo pia klabu ya Simba itakuwa kwenye dimba la sokoine katika mtanange dhidi ya Mbeya na Azam itakipiga na Stand utd.

Comments