Timu ya Yanga imeendelea kutamba ligi kuu Vodacom baada kuichapa Mbao FC bao 3-0.
Yanga ilifunga mabao hayo kipindi cha pill kupitia Vicent Bossou, Amis Tambwe na goli lingine likiwa la kujifunga baada ya golikipa wa Mbao FC Emanuel Semwaza kushindwa kuuweka mkononi mpira uliorushwa na Mbuyu Twitte.
Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe ambaye amefunga bao la 3 leo amefikisha jumla ya goli 7 alizofunga msimu huu akiwa ameachwa bao 1 na Shiza Kichuya wa Simba.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kusogea kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 27 chini ya Simba yenye pointi 32.

Comments
Post a Comment