Yanga yaiacha Mtibwa mdomo wazi, Chirwa akitoa Gundu Taifa


Waliokuwa wanadhani Yanga inapotea huenda jana wamebaki na alama ya mshangao baada ya klabu hiyo kuondoka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Mshambuliaji Obrei Chirwa kwa mara ya kwanza alifunga bao lake la kwanza baada ya kuipataia Yanga bao la kuongoza, bao la pili lilifungwa na Simon Msuva na Donald Ngoma alihitisha kishindo cha ushindi wa Yanga baada kuweka bao la tatu nyavuni huku bao pekee la kufutia machozi kwa timu ya mtibwa likiwekwa nyavuni na Haruna Chanongo.

Pamoja na upinzani mkubwa uliooneshwa na Mtibwa Sugar ya Morogoro bado Yanga ilionekana kuwa imara na kuanzia sehemu ya ulinzi, kiungo na safu ya ushambuliaji hali iliyowapelekea kuondoka na pointi 3 kwenye mechi hiyo.

Comments