Zile tetesi za Pluijm kuachia nafasi ya ukocha Yanga hatimaye zaanza kutimia


Anayesadikika kuwa mrithi wa nafasi ya kocha wa Yanga Hans Der Pluijm, George Lwandamina hatimaye ametua jijini Dar es Salaam.

Ingawa jambo hilo linafanywa siri kubwa katika timu ya Yanga lakini kamati ya timu hiyo imependekeza kocha huyo wa zamani wa Zambia (Chipolopolo) kuwanoa wababe hao wa jangwani.

Zipo taarifa kuwa huenda Yanga wamemaliza kila kitu na kocha huyo na muda wowote kuanzia sasa ataingia rasmi kazini.

Lwandamina amewahi kuwa kocha bora mwaka 2014/15 wakati akiiona Zesco ya Zambia kwa mafanikio makubwa.

Comments