Chelsea watibua rekodi ya Spurs, waichapa Spurs 2-1.


Timu ya Chelsea jana ikiwa katika uwanja wa Stamford Bridge iliweza kutoka kifua mbele baada ya kupata ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Spurs.

Licha ya Spurs kupata bao la kuongoza na kutawala mchezo katika kipindi cha kwanza lakini Chelsea iliweza kuchomoa hilo kupitia Pedro na lile la ushindi likifungwa na Victor Moses kipindi cha pili.

Ushindi wa Chelsea umetibua rekodi ya Spurs ambao hawakupoteza mechi yoyote tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu.

Chelsea imejikita kileleni kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 31 ikifuatwa na Liverpool pamoja na Manchester city ambazo zote kwa pamoja zina pointi 30.

Comments