Conte aipigia saluti EPL


Kocha wa Chelsea Antonio Conte amekubali kuwa ligi ya England ndiyo ligi ngumu kuliko ligi zote barani Ulaya.

Conte alisema kuwa timu za England zina ushindani wa hali juu ikiwa ni pamoja na kuonesha soka zuri ziwapo uwanjani.

"Ni ligi ambayo unahitaji kujipanga na kuwandaa wachezaji wako kwa ajili ya kupambana wakati wote, kuna wakati unaweza kuongoza 1-0 au 2-0 lakini kwenye ligi hii hayo matokeo ni ya wazi kabisa muda wowote unaweza kushangaa vinginevyo.

" Nilianza na 4-2-4 lakini mambo hayakuwa mazuri kwa upande wetu lakini mfumo wangu wa sasa 3-4-3 umeleta matokeo bora tangu nilipoanza kutumia uwanjani."

Pia kocha huyo alisifu uwezo wa mchezaji wake Eden Hazard ambaye amerudi kwenye kiwango chake tangu kuanza kwa msimu wa 2016/17.

Comments