Gerrard astaafu rasmi kucheza soka


Aliyekuwa shujaa wa Liverpool Steven Gerrard ameachana rasmi na soka rasmi baada ya kutangaza kustaafu.

Gerrard mwenye miaka 36, ameamua kuachana rasmi na soka baada kusakata kabumbu kwa muda wa miaka 19.

Nahodha huyo wa zamani wa Liverpool na England huenda akajikita na masuala ya ukocha na tayari Liverpool imeanza taratibu za kumkabidhi timu ya vijana.

Shujaa huyo namba mbili wa Liverpool baada ya Ken Daglish ameiandikia Liverpool mafanikio baada ya kuipa taji la ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2005, kombe la ligi pamoja na FA Mara 2.

Comments