Mshambuliaji wa Arsenal Oliver Giroud ameinusuru timu yake kuchezea kichapo katika uwanja wa Old Trafford baada ya kuchomoa bao.
Giroud aliyeingia dakika za jioni alichomoa bao hilo dakika 87 ya mchezo baada ya kufunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Oxlade Chamberlain.
Matokeo hayo yamempa ahueni kocha Arsene Wenger ambaye timu yake ilipotezwa na Man utd katika eneo la katikati lililotawaliwa vema na Ander, Herrera, Michael Carrick na Paul Pogba.

Comments
Post a Comment