Hazard: City na Liverpool ndiyo wapinzani wetu


Kiungo mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard amesema kuwa ana hofu na Man city pamoja na Liverpool kuwa kikwazo kwenye mbio za ubingwa.

Chelsea inaongoza kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 31, Livepool na City zote zikiwa na pointi 30.
Hazard alisema kuwa timu hizo kwa sasa ziko vizuri na zinaleta ushindani mkubwa kwenye ligi ya England msimu huu.

"Wote wako vizuri msimu huu tunahitaji kucheza vizuri ili kuendelea kuwa juu yao.

" Wana wachezaji bora kwa mfano De Bruyne Manchester city na Phelipe Coutinho Liverpool." Alisema Hazard

Chelsea itakuwa na kibarua kizito cha kupambana na Manchester city ndani ya wikiendi hii katika uwanja wa Etihad.

Comments