Herrera: tunainjoi chini ya Mourinho


Kiungo wa Manchester united Ander Herrera amesema kuwa wachezaji wa Manchester united wana furaha juu ya maisha mapya na kocha wa sasa Jose Mourinho.

Herrera mwenye miaka 27, alisema kuwa 
wanachezaji wote wana amani na furaha kikosini tangu alipotua Jose Mourinho.

"Mimi najisikia furaha na faraja kucheza chini ya Jose Mourinho, hakuna jambo gumu nina imani kila mmoja anayo furaha.

" Kila mmoja anamwona kocha wetu ni mkombozi wa timu hii kwa ujumla tuna imani naye." Alisema

Dau la £89.5 la usajili wa kiungo Paul Pogba limezua mjadala kutokana na utd kusua sua kurejea katika kiwango tangu Mourinho alipoakabidhiwa rungu la usajili na matajiri hao wa familia ya Glazers.

Comments