Liverpool yakamata usukani wa EPL, yaichapa Watford 6-1.


Timu ya Liverpool imeendelea kutishia amani katika ligi ya EPL baada ya jana kuichapa Watford bao 6-1 katika uwanja wa Anfield.

Mabao ya Liverpool yaliwekwa nyavuni na Sadio Mane ambaye alifunga mara mbili, Phelipe Coutinho, Roberto Firmino, Emre Can na Giorginio Wijnaldum.

Liverpool imekusanya pointi 26 ikiziacha Manchester city, Arsenal ambao wote walitoa sare katika michezo iliyopita na Chelsea ikiachwa pointi moja na vijogoo hao wa Anfield baada ya kuiburuza Everton bao 5-0.

Liverpool imekuwa tishio zaidi msimu huu kutokana na wachezaji wake kuwa na kasi kubwa uwanjani ikiwa ni pamoja na kutengeneza nafasi nyingi za magoli.

Comments