Manara: Simba haitakubali mwamuzi wa ndani dhidi ya Yanga


Timu ya Simba kupitia msemaji wake Haji Manara imesema kuwa haitakubali tena mwamuzi wa ligi za ndani kuamua katika mechi dhidi ya watani wa jadi.

Awali Simba haikuridhishwa na kile kilichotokea katika mechi yao ambayo ilipata sare ya bao 1-1 dhidi ya Yanga katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu.

Simba imeweka wazi msimamo wao kuwa haitakubali mwamuzi wa ndani kuamua mechi kutokana na kile kilichofanywa na 
Martin Saanya ambaye ambaye alikataa goli la sahihi la Ibrahimu Ajib pamoja na makosa mengine.

"Nadhani hatuna sababu ya kutumia mwamuzi wa ndani endapo tutakutana na Yanga kwa Mara nyingine". Alisema Manara.

Comments