Mabingwa wa Congo DRC TP Mazembe jana wametwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho baada ya kuichapa Mo Bejaia jumla ya mabao 5-2.
Jana kwenye uwanja wa nyumbani jiijini Lubumbashi TP Mazembe iliweza kuibuka na ushindi wa bao 4-1 na kunyanyua kombe hilo.
Awali TP Mazembe ilipata sare katika mchezo uliofanyika Algeria kwenye uwanja wa MO Bejaia ambapo timu hizo zilitoka 1-1.
Huu ubingwa wa kwanza kwa TP Mazembe kwenye kombe hilo licha ya kutwaa taji la klabu bingwa Afrika mara tano.

Comments
Post a Comment