Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale ameanza kuingia rasmi kwenye dunia ya wana michezo matajiri duniai baada ya waajiri wake Real Madrid kumtengea mshahara wa pauni 600,000 kwa wiki.
Bale atamfunika nyota wa Ureno Christiano Ronaldo ambaye anaondoka na kitita cha Pauni 290000 kwa wiki baada ya makato ya kodi ikilinganishwa na Bale ambaye ataondoka na kitita cha pauni 350000 .
Mshahara huo wa Gareth Bale huenda ukavunja rasmi matumaini ya Manchester united kumsajili nyota huyo hapo mwakani.
Bale anatarajiwa kusaini mkataba mpya ambao utamuweka Santiago Bernabeu hadi mwaka 2022 akiwa ni mchezaji wa nne kujitia kitanzi kwenye timu hiyo baada ya Tony Kroos, Luca Modric na Lucas Vazquez.

Comments
Post a Comment