Neymar, Coutinho waisambaratisha Argentina, yapigwa 3-0.


Timu ya Argentina imeendelea kuwa mteja wa timu ya taifa ya Brazil baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0.

Katika mechi hiyo ya kuwania tiketi ya kufuzu fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Russia, Brazil ilijipatia magoli ya ushindi kupitia Neymar, Coutinho na kiungo anayecheza ligi ya China Paulinho.

Mshambuliaji wa Barcelona Neymar amefikisha jumla ya magoli 50 katika timu ya taifa baada ya kufumania nyavu mara moja kwenye mechi hiyo.

Comments