Ngoma aikingia kisogo Yanga, huenda akatimka majuu


Licha ya kufanya vizuri na timu ya Yanga mshambuliaji Donald Ngoma amegoma kuongeza mkataba kwenye timu hiyo.

Mkataba wa Ngoma unamalizika mwisho wa msimu huu tangu alipotua kwenye timu hiyo mwaka jana.

Mchezaji huyo ambaye ni gumzo kwa mabeki wa ligi kuu nchini huenda akatimka kwenye moja ya klabu zenye ushindani katika bara la Ulaya.

Ngoma alieza kuwa ushindani mdogo ndiyo katika ligi ya Vodacom umemfanya kuchukua maamuzi ili kutengeneza mafaniko zaidi katika soka.

Ngoma amekuwa na kiwango bora tangu alipojiunga na Yanga akitokea Platinum ya nchini Zimbabwe.

Comments