Niyonzima, Msuva waing'arisha Yanga Uhuru


Mabingwa watetezi wa ligi kuu Vodacom Yanga wamemaliza salama raundi ya kwanza ya ligi kuu kwa ushindi baada ya kuichapa Ruvu shooting bao 2-1.

Ruvu Shooting ilianza kupata bao la kuongoza lakini hata hivyo Yanga ilichomoa kupitia Simon Msuva na kufunga la ushindi kupitia Haruna Niyonzima.

Matokeo hayo yameiongoza Yanga kusimama kwa pointi 33 ikiachwa pointi 2 na Simba ambayo ilipoteza mechi ya jana.

Comments