Kocha wa Simba Joseph Omog amesema kuwa mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe ndiye mshambuliaji hatari zaidi ligi kuu.
Omog alisema kuwa Tambwe anahitaji ulinzi wa kutosha kwa kuwa anaweza kufunga muda wowote akiwa uwanjani.
Licha ya kumwaga Sifa za mshambuliaji huyo, kocha huyo aliongeza kuwa anatamani kufanya kazi na Tambwe ambaye aliwahi kuitumikia simba misimu 3 iliyopita.
"Tambwe ni mshambuliaji hatari uwanjani ni vizuri kuimarisha ulinzi akiwepo kwa kuwa anaweza kufunga goli muda wowote.
"Ikitokea nitakuwa tayari kufanya kazi na Tambwe siku moja ni mshambuliaji hatari ambaye analijua goli." Alisema Omog.

Comments
Post a Comment