Pluijm aicha vizuri Yanga, ni baada ya kumaliza na ushindi dhidi ya Ruvu Shooting


Kocha Hans van der Pluijm ndiyo ameiga rasmi Yanga hapo jana ni baada ya kuichapa Ruvu Shooting kipigo cha mabao 2-1.

Rasmi Pluijm anaachana na timu Yanga baada ya aliyekuwa kocha wa ZESCO George Lwandamina kuvunja mkataba na timu yake ili kutua kwa wababe hao wa jangwani.

Katika kipindi cha miaka miwili kocha Mholanzi huyo ameingoza timu hiyo kutwaa mataji mawili ya ligi kuu, kombe la shirikisho na kuiongoza Yanga kwenye makundi michuano ya shirikisho barani Afrika.

Kocha anaicha Yanga ikiwa imemaliza salama mzunguko wa kwanza zikiwa zimebaki pointi mbili pekee kumfikia mpinzani wao Simba ambaye anaongoza kwa pointi 35 hadi sasa ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 33.

Comments