Sanchez awatoa hofu mashabiki wa Arsenal


Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez atakuwa fiti kuikabili  Manchester united wikiendi hii.

Sanchez ambaye afya yake ilikuwa kwenye utata kutokana na majeraha amerejea uwanjani baada ya jana kuingoza  Chile  katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Uruguay.

Katika mechi hiyo Sanchez alifunga mabao mawili na kutangaza habari njema kwa mashabiki wa Arsenal waliokuwa na wasi wasi kuhusiana na afya ya mchezaji hiyo.

Kurudi kwa Sanchez kumeinua matumaini kwa mashabiki wa Arsenal ambao timu yao itakaribishwa Old Trafford na Man utd.

Comments