Uongozi wa Simba umefunga kelele za ushindani kuhusu hatma ya usajili wa beki wao wa kushoto Mohammed Zimbwe baada ya kumalizana nae jana.
Zimbwe Jr maarufu kama Tshabalala amekamilisha makubaliano yake na Simba ambayo ilimaliza suala la Zimbwe mbele ya meneja wake Herry Mzozo.
Beki huyo ambaye alikuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Yanga sasa ataendelea kuitumikia Simba baada kuongeza miaka 2 kwenye mkataba wake.
Mbali na kushughulikia usajili wa
Tshabalala Simba inakutana leo kumaliza suala la mkude ambaye pia amehusishwa kujiunga na Yanga tangu kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili.
Heka heka za usajili zimezid kushika kasi Tanzania bara katika timu mbalimbali ikiwemo Azam ambayo tayari imefanikiwa kusajili washambuliaji wawili kutoka Ghana.

Comments
Post a Comment