Simba yakalishwa na African Lyon, yapigwa 1-0.


Timu ya simba leo imepata mbabe waketangu kuanza kwa msimu huu baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa African Lyon.

Simba haikupoteza mechi yoyote tangu kuanza kwa msimu ambapo leo imefungua ukarasa mwingine na kushindwa kuendelea na rekodi yao ya kutopoteza pointi 3.

Kwa matokeo hayo kunaifanya simba kukomea kwenye pointi 35 bado ikiwa kileleni kwenye msimamo wa ligi kuu ya Vodacom.

Kwa upande mechi nyingine mkoani Mbeya Yanga imeondoka na pointi 3 baada ya kuifunga Prisons bao 1-0  katika uwanja wa Sokoine.

Comments