Simba yakalishwa tena Sokoine, yapigwa 2-1 na Prisons


Timu ya Simba imeanza kuonja joto ya jiwe ligi kuu baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons leo katika uwanja Sokoine.

Simba imepoteza pointi 6 katika michezo miwili mfululizo ambapo wiki iliyopita wana msimbazi hao walikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa African Lyon.

Simba ndiyo iliyoanza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia Jamal Mnyate, hali iliyowafanya Prisons kurudi kwa kasi kipindi cha pili ambapo walichomoa bao na kuongeza bao la ushindi.

Matokeo hayo yanaongeza shangwe katika mitaa ya Jangwani ambao endapo watashinda mechi yao dhidi ya Ruvu Shooting wataisogelea Simba nyuma kwa pointi mbili.

Hadi sasa Simba ina jumla ya pointi 35 na kama Yanga itaondoka na pointi 3 dhidi ya Ruvu Shooting bila shaka itakuwa imepunguza jumla ya pointi 6 kwa Simba.

Comments