Timu ya Simba imevunja rekodi ya Stand united baada ya kuichapa bao 1-0 katika uwanja wa Kambarage.
Stand ambayo haikuwahi kupoteza mechi msimu huu imesalimu amri kwa Simba ambayo ilipata bao la ushindi kupitia Shiza Kichuya aliyefunga kwa mkwaju wa penati.
Ushindi huo unaiongoza Simba kuongoza ligi kuu kwa pointi 35 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 27 ambayo imepoteza mechi ya leo dhidi ya Mbeya City.

Comments
Post a Comment