Sturridge achungulia mlango wa kutokea Liverpool


Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge huenda akatimka Anfield kwenye dirisha dogo la usajili January.

Sturridge mwenye miaka 27 ameshindwa kumshawishi Jurgen Klopp kutumia kwenye kikosi cha kwanza mbele ya mbrazil Roberto Firmino.

Firmino ambaye anaonekana kufiti kwenye mfumo wa Jurgen Klopp anaweza kuwa sababu kubwa ya kuondoka kwa Sturridge kwenye timu huyo.

Hadi sasa klabu kadhaa zinavutika na mpango wa kumsajili strika huyo ikiwemo Everton, West Ham na Watford

Licha ya kukosa kwenye kikosi cha kwanza cha Jurgen Klopp lakini bado mshambuliaji amekuwa na uwezo mkubwa wa kufumania nyavu uwanjani.

Comments