Timu ya Intermilan bado haijaachana na mpango wa kuinasa saini ya kiungo mshambuliji wa Chelsea Oscar.
Oscar ameshindwa kupata nafasi katika timu ya kwanza ya kocha Antonio Conte tangu alipoanza kutumia mfumo wa 3-4-3 baada ya kuyumba katika mechi za awali.
Huenda nyota akatimka Serie A mwezi January baada ya Conte kuweka wazi kuwa atampiga bei Mbrazil huyo endapo atapokea ofa ya kutosha.
mbali na Oscar huenda Cesc Fabrigas akatimka Serie A baada ya AC Milan na Juventus kuonesha nia ya dhati kumsajili mhispania huyo.

Comments
Post a Comment