Toure aiangukia Manchester city


Kiungo mstaafu wa Ivory Coast Yaya Toure ameomba msamaha kwa uongozi wa timu ya Man city ili kuondoa tofauti zilizopo baina yao.

Toure alikuwa na mgogoro na timu hiyo kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri  dhidi ya kocha wa sasa wa timu hiyo Pep Gurdiola ambaye aliwahi kumuweka sokoni nyota huyo alipokuwa nae Barcelona.

Kocha wa city Pep Gurdiola amesema kuwa kwa sasa mchezaji huyo atatumikia benchi hadi hapo wakala wa mchezaji huyo Dimitri Seluk atakapomuomba radhi kocha kutokana na kumtuhumu kumdhalilisha Yaya Toure.

Kauli ya wakala huyo ilikuja baada ya Gurdiola kumwacha Toure katika kikosi kitakachoshiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu.

Comments