Usain Bolt atangaza kutandika daluga kwenye riadha


Mwanariadha wa Jamaica anayetamba duniani kwa sasa Usain amesema kuwa ataachana na riadha baada ya mashindano yatakayofanyika London mwakani.

Bolt ambaye amenyakua medali 9 za dhahabu katika michezo mitatu ya Olympic alisema kitendo hicho kitakuwa ni cha heshima kubwa kwake.

"Nadhani nastahili kupumzika, pale unapokuwa na kila kitu unachokihitaji kwenye fani uliyonayo hutakiwi kujichosha.

"Niliwahi kumuuliza Michael Johnson John kwanini aliwahi kustaafu alinijibu na kuniambaia alihitaji kujenga heshima kutokana na mafaniko makubwa aliyokuwa nayo.
" Bila shaka mashindano ya London yatakuwa ya mwisho kwangu baada ya hapo nitaachana na rasmi na riadha."  Alisema Bolt.

Bolt amekuwa hashikiki kwenye mbio za 100 m na 200 m tangu alipoibuka rasmi kwenye fani kutokana na kasi yake kubwa kwenye riadha.

Comments