Klabu ya Azam imefanikiwa kusajili washambuliaji wawili kutoka Ghana Hapo jana.
Nyota hao ni Samwel Afful kutoka Sekondi Hasacaan pamoja na Yahaya Mohammed kutoka Aduana Stars zote za nchini Ghana.
Zoezi hilo lilishuhudiwa na viongozi wa Azam akiwemo mkurugenzi mtendaji wa timu hiyo Saad Kawemba, meneja wa Azam Abdul mohammed pamoja na kocha mkuu Zeben Hernandez.
Samwel Afful 20 aliyesainia miaka 3, ni kinda ambaye anaitumikia timu ya taifa ya vijana ya Ghana U23 ambayo ameichezea kwa mafanikio makubwa, pamoja na kuifungia timu ya Sekondi mabao 9.
Pia Yahaya Mohammed 28 ni moja kati ya washambuliaji wazoefu katika ligi ya Ghana ambapo msimu uliopita alikuwa wa pili kwa ufungaji baada ya kutupia nyavuni bao 17.
Picha na Tovoti ya Azam (azamfc.co.tz)

Comments
Post a Comment