Aliyekuwa beki wa Azam FC Serge Wawa ameachana na timu na sasa ameamua kurejea tena El Merreik ya Sudan.
Wawa amesaini miaka 2 ya kuitumikia timu hiyo ambayo awali alikuwa nayo kabla ya kusajiliwa na Azam FC.
Wawa ambaye alikuwa na wakati mzuri tangu alipotua Azam alianza kutetereka baada ya kuanza kukumbwa na majeraha ya Mara kwa Mara uwanjani.
Hata hivyo kocha Azam Zeben Hernandez alionesha kutizishwa na mwenendo wa mchezaji huyo hali iliyopelekea beki huyo kurejea alipokuwa.

Comments
Post a Comment